Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Agosti 02, 2021 Local time: 22:40

Messi akosekana kwenye vipimo vya  kuanza msimu mpya Barcelona


Lionel Messiya lashe Ballon d'Or sau 6

Ligi ya Hispania-La Liga siku ya Jumapili ilitoa taarifa ikisema mkataba wa mchezaji machachari wa Barcelona Lionel Messi bado ni halali, siku kadhaa baada ya taarifa yake kushtusha kwamba anataka kuondoka katika klabu hiyo na saa kadhaa baada ya kushindwa kuhudhuria vipimo vya kuanza msimu mpya .

Kukosekana kwa Messi kwenye vipimo kumeonyesha nia ya dhati ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 ya kuondoka katika klabu hiyo ambayo amekuwa nayo katika kipindi chake chote tangu aanze kucheza soka la kimataifa.


Messi aliyechukua tuzo ya mchezaji bora wa dunia mara sita anasisitiza ana kifungu katika kandarasi yake ambacho kinamruhusu kuondoka kama mchezaji huru madai ambayo yalipingwa na Barcelona na hivi sasa na yanapingwa pia na La Liga.


Baraza linaloongoza ligi hiyo lilisema njia pekee ya klabu nyingine kuweza kumsaini mshambuliaji huyo wa Argentina ni ikiwa atabadilisha kifungu cha kutolewa kwa Euro milioni 700.

Msimamo huo wa La Liga ni pigo kwa matumaini ya Messi ya kuondoka haraka na kwa vilabu vinavyotaka kumsaini.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG