Wakati Marekani na mataifa mengine, ikiwemo Canada, yametuma meli za kivita katika eneo hilo katika wiki za karibuni, na itakuwa ni mara ya kwanza kwa jeshi la Ujerumani kupita hapo toka 2002.
China inadai kuwa na mamlaka kwa Taiwan inayotawaliwa kidemokrasia, na inasema inamiliki takriban kilomita 180 za njia ya maji inayogawanya pande mbili ikiwa ni sehemu ya South China Sea.
Taiwan inapinga vikali madai ya mamlaka ya China na inasema watu wa kisiwa hicho pekee ndio wanaweza kuamua mustakabali wao.
Mlango wa bahari wa Taiwan ni njia kuu ya biashara ambayo karibu nusu ya meli za biashara ya kimataifa hupitia, huku Marekani na Taiwan zikisema ni njia ya kimataifa ya bahari.
Forum