Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 04:43

Meli yenye bendera ya Marekani yashambuliwa na wanamgambo wa Kihouthi


FILE - Wanamgambo wa Kihouthi wakiandamana kuwaunga mkono Wapalestina wa Ukanda wa Gaza and kupinga mashambulizi yanayofanywa na Marekani huko Yemen nje ya mji wa Sanaa, Jan. 22, 2024.
FILE - Wanamgambo wa Kihouthi wakiandamana kuwaunga mkono Wapalestina wa Ukanda wa Gaza and kupinga mashambulizi yanayofanywa na Marekani huko Yemen nje ya mji wa Sanaa, Jan. 22, 2024.

Wanamgambo wa Kihouthi wenye makao yao Yemen waliishambulia meli  ya makontena yenye bendera ya Marekani iliyokuwa inapita inapita katika Bahari ya Arabia Jumanne.

Shirika la United Kingdom Maritime Trade Operations linasema nahodha wa meli ya Maersk Sentosa aliripoti mlipuko uliotokea karibu na chombo hicho nje kidogo ya pwani ya Nishtun, Yemen.

Msemaji wa Kikundi hicho alitoa taarifa Jumanne usiku akidai kuhusika na shambulizi hilo dhidi ya meli ya Maersk Sentosa, pia mashambulizi yaliyolenga meli nyingine mbili zilizokuwa zinapita katika Ghuba ya Aden.

UKMTO inasema meli ya Maersk Sentosa na mabaharia wake wako salama.

Wahouthi wamekuwa wakifanya mashambulizi ya droni na makombora dhidi ya meli za biashara katika Bahari ya Sham na Ghuba ya Aden tangu Novemba 2023, wakisema wanafanya hivyo kuonyesha mshikamano na Wapalestina wakati vita vya Gaza vikiendelea,

Kampeni yao imekuwa ikiyumbisha safari za meli za biashara zinazopita katika njia muhimu, na kusababisha makampuni mengi kubadilisha njia ya safari za meli kuchukua njia ndefu na gharama kuzunguka bara la Afrika.

Majeshi ya Marekani na Uingereza yamefanya mashambulizi ya anga dhidi ya malengo kadhaa ya Wahouthi huko Yemen. Wahouthi walisema watu 16 waliuawawa na kiasi cha darzeni tatu wengine walijeruhiwa katika mfululizo wa mashambulizi ya anga Mei 30.

Wakati huo huo, zaidi ya darzeni mbili ya wafanyakazi wa kimataifa, wakiwemo wafanyakazi kadhaa kutoka Umoja wa Mataifa, wamezuiliwa na waasi wa kihouthi tangu katikati ya mwezi Juni, wakiwemo wafanyakazi 18 waliokamatwa baada ya upekuzi uliofanyika mara kadhaa Julai 4.

Baadhi ya taarifa hii inatokana na ripoti za mashirika ya habari ya AP, na Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG