Ilikuwa ni moja ya uingiliaji kati mkubwa zaidi katika miezi ya karibuni kwa wahamiaji wanaotafuta maisha bora barani Ulaya kupitia nchi hiyo iliyokumbwa na vita ya Kaskazini mwa Afrika.
Walinzi wa pwani walisema boti hiyo ilisimamishwa Ijumaa karibu na mji wa Mediterranean wa Moura, kiasi cha kilomita 90 magharibi mwa mji wa mashariki mwa Libya wa Benghazi.
Katika taarifa yao amesema kwamba wahamiaji hao wanatoka mataifa tofauti na kwamba wale walioingia kinyume cha sheria nchini Libya watakabidhiwa kwa nchi zao. Taarifa hiyo haikutoa maelezo zaidi.
Walinzi wa pwani walibandika picha kwenye mtandao wa Facebook zikionyesha boti kubwa iliyojaa watu wengi kupita kiasi huku wengi wa waliokuwemo humo wakionekana kuwa vijana.