Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 03, 2024 Local time: 23:16

Meja jenerali Haliva wa Israel ametangaza kujiuzulu wadhifa wake


 Meja jenerali Aharon Haliva wa Israel
Meja jenerali Aharon Haliva wa Israel

Aharon Haliva ni afisa wa kwanza wa ngazi ya juu Israel kujiuzulu kuhusiana na shambulio la oktoba 7 la hamas dhidi ya Israel.

Jeshi la Israel limetangaza kujiuzulu kwa mkuu wa idara yake ya upelelezi kujibu shambulio la Oktoba 7 la Hamas dhidi ya Israel.

Meja Jenerali Aharon Haliva tayari alitangaza hadharani jukumu la kushindwa kwa upelelezi uliosababisha shambulio ambapo Israel inasema wanamgambo wa Hamas waliwaua watu 1,200 na kuwateka nyara watu 250.

Jeshi leo Jumatatu lilitoa barua ya kujiuzulu kutoka kwa Haliva na kusema ataondoka katika wadhifa wake na kustaafu mara tu mtu atakayechukua nafasi yake atakapoteuliwa. Kurugenzi ya upelelezi chini ya uongozi wangu haikutimiza wajibu tuliokabidhiwa.

Ninaibeba siku hiyo nyeusi tangu wakati huo, siku baada ya siku. Nitayabeba maumivu haya milele, Haliva alisema katika barua hiyo. Haliva ni afisa wa kwanza wa ngazi ya juu kujiuzulu kuhusiana na shambulio hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG