Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 02:32

Meghan na Prince Harry wailaumu familia ya kifalme ya Uingereza


Prince Harry (kushoto) na mkewe Meghan, wakiwa katika mahojiano ya televisheni na Oprah Winfrey. - March 7, 2021…

Meghan Merkel mke wa Prince Harry ameilaumu familia ya kifalme ya Uingereza kwa kuzua wasi wasi kutokana na rangi ya mwanaye swali llilompelekea kutafakari kuhusu kujitoa uhai.

Hayo ameyasema wakati wa mahojiano Jumapili, swala ambalo huenda likazua hali ya taharuki kwenye familia ya kifalme ya Uingereza.

Meghan mwenye umri wa miaka 39 na ambaye ni mweusi anasema kuwa hakufikiria suala la rangi kabla ya kuolewa mwaka 2018.

Anasema kuwa alitafakari kujitoa uhai baada ya kuomba msaada kutoka kwa wanafamilia wa kifalme, lakini hakuna aliyemsaidia.

Ameongeza kusema kuwa mwanaye Archie ambaye sasa ana umri wa mwaka mmoja alinyimwa jina la prince kwa kuwa baadhi ya wanafamilia walimuona akiwa mwenye ngozi nyeusi mara baada ya kuzaliwa.

Kwenye mahojiano hayo na Oprah Winfrey kupitia televisheni ya CBS, Meghan alisema kuwa alipata ujumbe huo kutoka kwa mume wake Harry baada ya kuwa na kikao na wanafamilia.

Wawili hao baadaye walijiondoa kwenye familia ya kifalme na badala yake kuamua kuishi hapa Marekani kama watu wa kawaida.

XS
SM
MD
LG