Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 05, 2023 Local time: 17:40

Mdahalo wa kugombania kiti cha rais Uganda utafanyika


Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika picha
Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika picha

Baraza la dini mbali mbali la Uganda linaeleza kuwa mdahalo wa mwisho wa wagombea urais kabla ya uchaguzi mkuu nchini humo utaendelea kama ulivyopangwa kufanyika Februari 13.

Kulikuwa na taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari nchini humo kwamba rais Yoweri Museveni hatoudhuria .

Maafisa wa taasisi hiyo wanasema wako kwenye mazungumzo na chama cha NRM kuhakikisha kwamba rais Museveni anashiriki mdahalo huo.

Mdahalo huo umelenga kuwapa wapiga kura watarajiwa kupata nafasi ya kuchagua mgombea yupi ana sera bora za kuweza kuondoa changamoto zinazoikabili nchi .

Vile vile mdahalo huo utalenga kutolewa maelezo ya kukabiliana na changamoto za nchi hiyo , uhusiano wa kikanda ,usalama na Amani , biashara ya kimataifa na uwekezaji.

Wagombea wote nane wamealikwa kushiriki katika mdahalo huo wa pili na wa mwisho kabla ya kufanyika uchaguzi wa rais, bunge na serikali za mitaa.

Lakini baadhi ya waganda wanasema kwa kiasi kikubwa wanaamini Museveni hatatokea kama ilivyokuwa katika mdahalo wa kwanza.

XS
SM
MD
LG