Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 23:41

Mdahalo wa kwanza wa wagombea urais Marekani


Wagombea urais wa Republican kutoka kushoto, Chris Christie, Marco Rubio, Ben Carson, Scott Walker, Donald Trump, Jeb Bush, Mike Huckabee, Ted Cruz, Rand Paul, na John Kasich.
Wagombea urais wa Republican kutoka kushoto, Chris Christie, Marco Rubio, Ben Carson, Scott Walker, Donald Trump, Jeb Bush, Mike Huckabee, Ted Cruz, Rand Paul, na John Kasich.

Wagombea urais 10 wa chama cha Republican walio katika nafasi ya juu walizindua rasmi msimu wa kampeni mwaka 2016 kwa mdahalo wao wa kwanza uliofanyika Alhamis usiku huko Cleveland, katika jimbo la Ohio.

Licha ya mikwaruzano kwa njia moja au nyingine lakini mdahalo ulifikia matakwa yaliyotarajiwa. Bilionea Donald Trump alieleza kwamba hadhani kama atashindwa na kwamba ana shauku ya kujibu mashambulizi.

Donald Trump
Donald Trump

Lakini matamshi yaTrump huwenda yalizua khofu miongoni mwa baadhi ya wa- Republican kuhusu nia yake ya dhati katika chama. Trump alikuwa mgombea pekee jukwaani ambaye alikataa kukubali kumuunga mkono mgombea yeyote atakayeteuliwa na chama cha Republican kuwania kiti cha urais na kuelezea uwezekano wa kuwa mgombea binafsi wa urais.

Donald Trump alisema “sitaweka ahadi kwa wakati huu” pale alipoulizwa swali na mmoja wa waendeshaji mdahalo huo.

XS
SM
MD
LG