Upatikanaji viungo

Mchungaji auawa kanisani Mombasa


Kenya imeshambuliwa mara kadhaa kwa matukio yanayohusishwa na ugaidi ikiwemo la Westgate mall

Watu wenye silaha wasiofahamika walimfyatulia risasi na kumuuwa mchungaji mmoja wakati wa ibada kanisani siku ya jumapili katika mji wa Mombasa nchini Kenya maahala ambako polisi wanapambana na vijana wa ki-islam wenye msimamo mkali.

Mauaji hayo yalitokea ndani ya mlango mkuu wa kuingilia kwenye kanisa la Maximum Revival Centre katika mtaa wa majengo. Mashahidi wanasema polisi waliwazuia watu wenye silaha kuingia ndani ya kanisa na kuuwa waathirika Zaidi.

Watu hao wenye silaha hawajafahamika lakini kundi la wanamgambo wa Al-Shabab kutoka nchi jirani ya Somalia limeshambulia malengo kadhaa nchini Kenya. Kundi hilo la Al-Shabab liliapa kulipiza kisasi kwa majeshi ya Kenya kuwepo nchini Somalia kwa ajili ya kusaidia wanajeshi wa serikali dhidi ya wanamgambo hao.

XS
SM
MD
LG