Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 20, 2023 Local time: 18:44
VOA Direct Packages

Mcheza soka wa kimataifa kutoka Ghana apatikana akiwa amekufa kutokana na tetemeko la ardhi la Uturuki


Christian Atsu aliyepatikana akiwa amekufa chini ya vifusi vya jengo, Uturuki.

Wakala wa Uturuki wa mcheza  soka maarufu kutoka Ghana aliyewahi kuichezea timu ya Chelsea Christian Atsu amesema kwamba amepatikana akiwa amekufa chini ya vifusi vya jengo lililoporomoka kusini mwa Utruki kufutia tetemeko la ardhi la hivi karibuni.

Murat Uzunmehmet amewaambia wanahabari mjini Hatay ambako mwili wake ulipatikana, kwamba baadhi ya vitu vyake pia vimepatikana, ikiwepo simu yake. Ripoti zimeongeza kusema kwamba Atsu alikuwa aondoke kusini mwa Uturuki saa chache kabla ya kutokea kwa tetemeko hilo lakini akaamua kubaki kidogo pamoja na wachezaji wenzake baada ya kupata goli la ushindi kwenye mechi ya Super Lig hapo Februari 5.

Wizara ya mambo ya nje ya Ghana imesema kwamba ndugu yake pamoja na dada yake pacha walikuwepo wakati mwili huo ukigunduliwa. Ubalozi wa Ghana unaendelea na mipango za kuurejesha nyumbani wa ajili ya mazishi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG