Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 25, 2024 Local time: 20:24

Kikosi cha mbwa cha Kenya kupambana na ujangili


Nchi kadhaa Jumapili ziliadhimisha Siku ya Mazingira Duniani ambayo kauli mbiu mwaka huu ikiwa ni kupambana na biashara haramu ya wanyama pori ya dola bilioni 20.

Huko Afrika Mashariki, timu mpya ya mbwa wakupambana na ujangili imejiunga katika kampeni hiyo.

Mbwa ajulikanaye kama Asha anafanya kazi akinusa masanduku katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi.

Asha amefunzwa kunusa pembe za ndovu katika viwanja vya ndege na bandari nchini Tanzania na Kenya akiwa ni sehemu ya timu mpya ya mbwa 8 wa kupambana na biashara haramu ya pembe za ndovu waliofunzwa na 'African Wildlife Foundation' wakishirikiana na Shirika la Wanyamapori la Kenya na lile la Tanzania. Mbwa wengine 8 watapelekwa Msumbiji na Uganda.

XS
SM
MD
LG