Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 19:18

Mbunge Wa Uganda Awekwa Mbaroni Kwa Msimamo Wa Kisiasa


Polisi wa Uganda
Polisi wa Uganda

Polisi wa Uganda wamemtia mbaroni mbunge mmoja na 10 wengine ambao walikamatwa wakati wakiandamana dhidi ya mpango ambao utamuwezesha rais wa muda mrefu nchini humo Yoweri Museveni kutawala maisha.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press-AP Emilian Kayima msemaji wa polisi katika mji mkuu Kampala alisema wanamshikilia mwanachama maarufu wa upinzani ambaye pia ni mbunge na wengine walioshutumiwa kukutana kinyume cha sheria siku ya Jumatatu.

Darzeni za wabunge wa chama tawala nchini humo walisema wiki iliyopita kwamba wataunga mkono muswaada wa kufuta kipengele cha umri kwenye katiba ya Uganda ambayo inamzuia mtu yeyote mwenye umri wa miaka 75 na kuendelea kutowania urais.

Rais Yoweri Kaguta Museveni.
Rais Yoweri Kaguta Museveni.

Rais wa Uganda Museveni ambaye alifikisha miaka 73 wiki iliyopita hastahili kuwania tena nafasi hiyo kama kipengele cha umri kitaendelea kuwepo ndani ya katiba. Rais Museveni amekuwepo madarakani katika taifa hilo la Afrika mashariki tangu mwaka 1986.

XS
SM
MD
LG