Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 21, 2024 Local time: 19:46

Mazungumzo ya Sudan Kusini na Kaskazini yaendelea


Kiongozi wa Sudan kusini Salva Kiir akiwasili Addis Ababa.
Kiongozi wa Sudan kusini Salva Kiir akiwasili Addis Ababa.

Mazungumzo yanaendelea huko Ethiopia kati ya Sudan Kusini na Kaskazini wakati Sudan Kusini ikijiandaa na uhuru wake jumamosi.

Viongozi wa Sudan Kusini na kaskazini wanakutana huko Ethiopia kuongelea masuala muhimu kadhaa ambayo hayajapata suluhu wakati Kusini ikijiandaa na uhuru wake jumamosi.

Rais wa Sudan Omar Al Bashir na kiongozi wa Kusini Salva Kiir wanafanya mkutano huo Jumatatu mjini Addis Ababa wakati pande hizo mbili zikifanya kazi kutafuta makubaliano juu ya kutumia pamoja rasilimali, sehemu za mpakani zenye mzozo na uraia.

Mkutano huo umekuja katikati ya wiki za mapigano katika jimbo tete la Kordofan Kusini na jimbo jirani la Abyei, ambayo yamesababisha kukimbia kwa kiasi kikubwa cha watu na wasi wasi wa kuingia tena kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Bw.Bashir amesema ameliamuru jeshi lake la kaskazini kuendelea na mapigano huko Kordofan Kusini kwa wakati wote ambao waasi bado wapo kwenye eneo hilo.

Maafisa wa jeshi la Sudan Kusini walisema jumapili kwamba mapigano hayo yanaweza kusambaa kwenye maeneo ya mpakani , kutoka Blue Nile mpaka Darfur endapo sitisho la mapigano halitatekelezwa.

XS
SM
MD
LG