Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 12:01

Mazungumzo ya Sudan Kusini yakwama


Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir akiingia katika mkutano wa mazungumzo ya amani baina ya Serikali yake na waasi.
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir akiingia katika mkutano wa mazungumzo ya amani baina ya Serikali yake na waasi.

Duru mpya ya mazungumzo ya amani baina ya makundi yanayopingana ya Sudan Kusini yamekwama hivyo kuondoa matumaini kwamba makubaliano yanaweza kufikiwa.

Serikali ya Sudan kusini na waasi wa upinzani wameshindwa kukutana katika mazungumzo yaliyopangwa kufanyika Addis Ababa alhamis kwa sababu ya shutuma za upinzani kuhusu taratibu za mashauriano hayo.

Pande zote mbili zilikubali kufanya mazungumzo ya amani na kumaliza mzozo uliozuka katikati ya mwezi Disemba ambapo mzozo wa kisiasa baina ya Rais Salva Kiir na mpinzani wake Riek Machar ulipogeuka na kuwa ghasia.

Kundi la upinzani limekataa kushiriki katika majadiliano siku mbili zilizopita likisema kuwa linataka kuzungumza moja kwa moja kumaliza ghasia kabla ya kujadili marekebisho ya kisiasa.

XS
SM
MD
LG