Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 10:54

Umoja wa Mataifa wafurahishwa na usitishaji mapigano nchini Yemen


Mwakilishi maalum wa UN kwa Yemen, Ismail Ould Cheikh Ahmed akizungumza na waandishi huko Sanaa, Yemen.
Mwakilishi maalum wa UN kwa Yemen, Ismail Ould Cheikh Ahmed akizungumza na waandishi huko Sanaa, Yemen.

Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Yemen, Ismail Ould Cheikh Ahmed, alikaribisha leo Jumatatu utaratibu wa kusitisha mapigano ambayo yamekuwepo zaidi ya mwaka mmoja akisema huu ni wakati wa kusafisha yaliyopita.

Makubaliano ya kusitisha vita kwa muda yalianza usiku kucha na serikali ya Yemen, ushirika unaoongozwa na Saudi Arabia ambao unaiunga mkono serikali na waasi wa kihouthi ambao walichukua udhibiti wa mji mkuu wa Yemen, mwishoni mwa mwaka 2014, wote wakiahidi kuheshimu makubliano.

Hatua hii inakuja kabla ya mazungumzo ya amani yaliyopangwa kufanyika April 18 nchini Kuwait. Ahmed amesema kuna fursa ya kweli ya kujijenga tena katika nchi ambayo imeathiriwa na ghasia kwa muda mrefu. "Ninaziomba vpande zote na jumuiya ya kimataifa kuendelea kuunga mkono utaratibu huu wa kusitisha mapigano ikiwa ni hatua ya kwanza katika kurejesha amani nchini Yemen," mwakilishi huyo alisema katika taarifa yake. Aliongeza kuwa hilo ni suala muhimu linalohitajika kwa haraka. Yemen haiwezi kumudu kupoteza maisha mengine ya watu.

XS
SM
MD
LG