Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 12:43

Mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini yaanza tena


Wapatanishi wa mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini mjini Addis Ababa Januari 13, 2014
Wapatanishi wa mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini mjini Addis Ababa Januari 13, 2014

Baada ya sherehe za ufunguzi rasmi, majadaliano hayo yatahamishiwa mji wa Debre Ziet, ulioko kilomita 45 kusini mwa Addis Ababa.

Mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini yanaanza tena Jumatatu mjini Addis Ababa Ethiopia, kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia Dina Mufti. Maafisa wanasema mara tu baada ya sherehe za ufunguzi rasmi, majadaliano hayo yatahamishiwa mji wa Debre Ziet, ulioko kilomita 45 kusini mwa Addis Ababa.

Mufti anasema pande zote mbili zinadai kuwa zinatii makubaliano ya kusitisha mapigano licha ya ripoti kwamba pande hizo zimekuwa zikipigana katika maeneo mbalimbali ya nchi.Na huku upinzani ukieleza tofauti zake na serikali inayoongozwa na chama cha SPLM, serikali ya Sudan Kusini nayo inasisitiza kuwa upinzani ulijaribu kuipindua.

Msemaji huyo wa wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia, anasema tofauti hizi kubwa zinahitaji kutanzuliwa ili mazungumzo yenye maana yaweze kuendelea. Anasema pia kuwa shirika la kikanda IGAD ambalo liliandaa maazungumzo hayo litaendelea kufuatilia kuona kwamba makubaliano ya kusitisha mapigano yanataekelezwa.

Timu ya ufuatiliaji tayari imepelekwa huko Sudan Kusini katika maeneo mbalimbali ya nchi. Pande zinazozozana zilitia saini makubaliano hayo Januari 4 kufuatia shinikizo la jamii ya kimataifa. Mtafaruku huo wa Sudan Kusini umesababisha vifo vya zaidi ya watu elfu moja na maelfu kulazimika kutoroka manyumbani mwao.

Serikali pia imewaachia huru wafungwa saba wa kisiasa kati ya 11 ambao walishtumiwa kwa jaribio la kupindua utawala wa Juba . Mufti anasema upinzani umeelezea kuwa wafungwa walioachiwa watakuwa sehemu ya majadiliano ya amani leo Jumatatu.
XS
SM
MD
LG