Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 26, 2023 Local time: 04:55

Mazungumzo ya amani ya Mashariki ya Kati yaanza Washington


Rais Obama anasema ni lazima kwa viongozi wa Israeli na Palestina kutumia nafasi ya mazungumzo ya ana kwa ana kufikia makubaliano ya amani ya kudumu huko Mashariki ya Kati.

Rais Barack Obama alikutana na kiongozi mmoja baada ya mwengine kutoka Israel, Palestina, Misri na Jordan katika White House kwa mara ya kwanza kwa majadiliano juu ya juhudi za kupatikana maendeleo katika masuala yaliyokuwa magumu kutanzuliwa na maraisi wa Marekani waliotangulia.

Katika moja kati ya vikao vitatu mbele ya waandishi habari akiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton, rais Obama alielezea baadhi ya masuala aliyomwambia Waziri Mkuu Benjamini Netanyahu na rais Abbas.

"Kama nilivyowaambia kila mmoja leo, nafasi hii iliyojitokeza huwenda isitokee tena. Hawawezi kuiachia nafasi hii itoweke. Sasa ni wakati kwa viongozi hao wenye ari na uwongozi wa kupatikana amani ambayo watu wao wanastahili", amesema Bw Obama.

Kiongozi huyo wa Marekani amesema lengo la mazungumzo ni kupatikana suluhisho la masuala yote ya hati ya mwisho, na makubaliano yatakayo fikiwa kwa mazungumzo yatakayopelekea kuundwa kwa taifa huru, litakaloweza kujitegemea la Palestin, likiishi kwa amani na usalama na jirani wake, taifa la Wayahudi la Israel.

Miongoni mwa masuala yanayojadiliwa tena katika mazungumzo ya ana kwa ana ni kuongezwa muda wa kusitishwa ujenzi wa makazi mepya ya walowezi huko Ukanda wa Magharibi, muda unaomalizika Septemba 26.

Waziri Mkuu Netanyahu, amesisitiza haja ya wa Palestina kuitambua Israel na kuhakikisha hatua za usalama wa kudumu na thabiti, pamoja na kumaliza ghasia. Kabla ya chakula cha jioni, viongozi wote watano walihudhuria mkutano na waandishi habari hapo White House, na kuelezea lengo lao kuu, ni kufikia makubaliano ya mwisho ya ugomvi kati ya Israeli na Palestina katika kipindi cha mwaka ujao.

XS
SM
MD
LG