Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 00:56

Mazungumzo baina ya serikali za Khartoum na Juba yaanza upya


Mwakilishi mkuu wa Sudan Kusini Pagan Amum
Mwakilishi mkuu wa Sudan Kusini Pagan Amum

Mpatanishi wa Sudan Kusini aeleza mashaka juu ya Khartoum

Afisa wa ngazi ya juu wa Sudan Kusini ameeleza mashaka yake juu ya nia ya dhati kutoka upande wa Sudan katika kutanzua mzozo baina ya nchi zao mbili huku duru mpya ya mazungumzo ikianza katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa. Katika mazungumzo yaliyoanza upya Jumanne mpatanishi mkuu wa Sudan Kusini Pagan Amum alisema upande unaowakilisha nchi yake unaingia kwenye mazungumzo hayo kwa nia safi. Alisema ni jukumu la maafisa wa Sudan kuonyesha kujitolea kwao kwa dhati kutanzua maswala nyeti yaliyovunja mazungumzo hayo mwezi jana. Katika mkesha wa mazungumzo hayo mapya serikali ya Khartoum ilitangaza kuwa itatii maazimio ya baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka iondoe wanajeshi wake kwenye eneo la Abyei linalozozaniwa. Sudan Kusini ilikuwa imeondoa askari polisi wake mia saba mapema mwezi huu. Mpatanishi mkuu wa Sudan Kusini Bw. Amum alisema timu yake itazindua duru hii mpya ya mazungumzo kwa kuorodhesha ukiukwaji wote uliofanywa na Khartoum katika maazimio ya baraza la Usalama na kwenye mpango maalum uliowekwa kutanzua maswala sugu yaliyosalia baada ya Sudan Kusini kuwa taifa huru rasmi Julai mwaka jana. Alisema orodha hiyo pia italijumwisha swala la Abyei. Vyombo vya habari vya Sudan vilinukulu msemaji wa jeshi la Khartoum akikanusha shtuma zote za Bw. Amum. Msemaji huyo aliitaka Juba kuthibitisha madai yake na kusema kuwa majeshi ya Khartoum kamwe hayahusiki na vurugu zinazoendelea Sudan Kusini. Wafuatiliaji wa kidplomasia wamesema jana kuwa ni vigumu kubashiri suluhu la haraka kwa sababu ya ugumu uliopo juu ya mswala yanayojadiliwa baina ya Sudan zote mbili . Miongoni mwayo mafuta na uraia.

XS
SM
MD
LG