Pentagon imesema Austin atakutana na kiongozi wa kijeshi wa China Dong Jun, watakapohudhuria mazungumzo ya “Shangri-La Dialogue” ya Mei 31 mpaka Juni 2, mkusanyiko wa kila mwaka wa maafisa wa ulinzi duniani kote.
China wiki hii iliizingira Taiwan kwa meli na ndege za kivita katika majaribio ya uwezo wake wa kukiteka kisiwa hicho, ambacho inadai ni himaya yake.
Mazoezi hayo yamefanyika baada ya kuapishwa Rais Lai Ching-te wa Taiwan, ambaye ameapa kulinda demokrasia ya taifa lake linalojitawala.
Mkutano wa Austin na Dong ulitarajiwa sana tangu walipozungumza kwa njia ya simu mwezi Aprili yakiwa ya kwanza kwa wakuu wa kwa takriban miezi 18.
Forum