Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 04, 2022 Local time: 06:18

Mawaziri wa Ulaya wakutana kujadili Ebola


Rais Barack Obama akizungumza baada ya kukutana na mawaziri wake walipojadiliana kuhusu Ebola

Mawaziri wa mambo ya nje wa Ulaya wanakutana huko Brussels kwa mazungumzo ya hali ya juu kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Ebola na jinsi ya kufanyia uchunguzi katika mipaka ya ulaya na viwanja vya ndege.

Mkutano wa Alhamisi umekuja siku chache baada ya uchunguzi mpya kufanywa katika viwanja vitano vya ndege nchini Marekani. Viwanja vyote vilivyoko katika miji mikubwa vinapata wasafiri wengi kutoka nchi za Guinea, Liberia, Sierra Leone zote za Afrika Magharibi ambako kuna mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.

Alhamisi wabunge wa Marekani watafanya mkutano na wataalamu wa juu wa afya kujadili vipimo vya Ebola na jinsi ya kudhibiti nchini Marekani.

Mkakati wa tiba ya ugonjwa wa Ebola imekuja kwa haraka baada ya wauguzi wawili wa huduma za afya kutoka jimbo la Texas kupata maambukizo ya ugonjwa huo wakati wakimtibu raia wa Liberia aliyekuwa amelazwa katika hospitali kwenye mji wa Dallas.

Jumatano iligunduliwa kwamba mmoja wa wafanyakazi walioathirika alipanda ndege ya abiria siku moja kabla ya kuanza kuonesha dalili za kuwa na ugonjwa huo.

Rais wa Marekani Barack Obama aliahirisha safari Jumatano ili kufanya mkutano wa dharura huko ikulu ya white house na mawaziri kuhusu ugonjwa wa Ebola.

XS
SM
MD
LG