Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 10, 2022 Local time: 07:45

Mawaziri wa Rwanda na DRC wakutana na Rais Joao Lourenco mjini Luanda kujadili kuendelea mapigano ya M23


Rais wa Angola Joao Lourenco akizungumza wakati wa mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa mjini Glasgow, Scotland.

Mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamekua na mazungumzo na rais Joao Lourenco mjini Luanda juu ya kuongezeka kwa uhasama na mapigano mashariki ya Congo.

Rais Lourenco, mpatanishi wa Umoja wa Afrika, amekutana na mawaziri Christophe Lutundula wa DRCongo na Vincent Biruta wa Rwanda baada ya kuongezeka kwa lawama wiki hii kati ya Kigali na Kinshasa, wakati wapiganaji wa kundi la M23 wakiendelea na mapigano na kuteka miji kadhaa ya mashariki ya Congo.

Luanda tayari imejaribu kupunguza mvutano kati ya majirani hao wawili mwezi wa Julai na makubaliano ya kusitisha uhasama yalifikiwa kati ya marais Paul Kagame wa Rwanda na Felix Tshisekedi wa Congo. Lakini kwenye uwanja wa mapigano hali haijabadilika.

Mvutano kati ya nchi hizo mbili ulianza kua mbaya mapema mwishoni mwa mwaka jana 2021 pale kundi la M23 lenya kuongozwa na watutsi wa Congo kuamua kuchukua silaha na kuanza kupambana na jeshi la taifa la Congo FRDC.

Kinshasa inadai Kigali inawasaidia M23 jambo ambao Rwanda inakanusha vikali.
Wiki hii Rais Felix Tshisekedi alilihutubia taifa na kuilaumu tena Rwanda na kuwataka wakongo wajiandikishe na jeshi ili kupambana na waasi wa mashariki.

Mapigano hayo yamekua makali mnamo wiki za mwisho za mwezi Oktoba na mapema mwezi wa Novemba pale M23 wamechukua udhibiti wa miji muhimu kama Rutshuru wakielekea mji wa Goma na kusababisha maelfu ya wakazi kukimbia kutoka vijiji na miji yao.

Kulingana na Umoja wa Mataifa mapigano kati ya FARDC na M23 yamewalazimisha watu elfu 50 kukimbia makazi yao tangu Oktoba 20, ambapo elfu 12 wameingia Uganda.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG