Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 21, 2024 Local time: 18:46

Mawaziri wa mambo ya nje wa EU wanatafakari vikwazo vipya kwa Russia


Rais wa Russia, Vladmir Putin
Rais wa Russia, Vladmir Putin

Umoja wa Ulaya tayari umeweka awamu nane za vikwazo vinavyolenga takwimu na viwanda vya Russia kujibu uvamizi wa Russia kwa Ukraine ulioanza mwezi Februari. Duru ya tisa itajumuisha maafisa wa serikali pamoja na viwanda vya ulinzi na benki vya Russia

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanatafakari vikwazo vipya dhidi ya Russia na fedha zaidi kulisaidia jeshi la Ukraine katika mkutano leo jumatatu, huku Marekani ikiahidi kuendelea kuiunga mkono Ukraine huku kukiwa na mashambulizi ya Russia dhidi ya miundombinu muhimu.

Mfuko uliopendekezwa wa EU unaojadiliwa huko Brussels utatoa karibu dola bilioni 2.1 kufadhili utoaji wa silaha kwa Ukraine.

Umoja wa Ulaya tayari umeweka awamu nane za vikwazo vinavyolenga takwimu na viwanda vya Russia kujibu uvamizi wa Russia kwa Ukraine ulioanza mwezi Februari. Duru ya tisa itajumuisha maafisa wa serikali pamoja na viwanda vya ulinzi na benki vya Russia.

Rais wa Marekani Joe Biden alizungumza na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy kwa njia ya simu Jumapili, moja ya mfululizo wa simu ambazo Zelenskyy alifanya na viongozi wa dunia kabla ya mazungumzo ya Umoja wa Ulaya na mikutano mingine muhimu wiki hii.

Taarifa ya White House imesema Biden "amethibitisha kujitolea kwa Marekani kuendelea kuipatia Ukraine msaada wa kiusalama, kiuchumi na kibinadamu, kuiwajibisha Russia kwa uhalifu wake wa kivita na ukatili, na kuiwekea Russia gharama kwa uvamizi wake."

XS
SM
MD
LG