Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 08:47

Mawaziri wa ASEAN kukutana India Alhamisi


Bendera za mataifa wanachama wa ASEAN kwenye mkutano wa awali wa Myanmar
Bendera za mataifa wanachama wa ASEAN kwenye mkutano wa awali wa Myanmar

Miaka minne iliopita, India ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa viongozi wa muungano wa mataifa ya kusini mashariki mwa Asia, ASEAN wakati wa maadhimisho ya kila mwaka ya gwaride la Jamhuri, hatua iliyoashiria ari ya taifa hilo ya kukuza muungano huo wenye wanachama 10.

Muungano huo unaonekana kuendelea kushamiri wakati mataifa mengine kama Marekani yakishirikiana na muungano huo katika kudhibiti ushawishi wa China kwenye eneo la Indo Pacific. Kuanzia Alhamisi, New Delhi itakuwa mwenyeji wa kikao cha siku mbili cha mawaziri wa mambo ya kigeni wa mataifa ya ASEAN, yakiwa maadhimisho ya miaka 30 ya ushirikiano wao wakati wakizungumzia ushirikiano zaidi.

Mwaka huu wa 2022 umetengwa kama mwaka wa urafiki wa India na ESEAN. Mataifa wanachama wa ASEAN ni pamoja na Singapore, Thailand, Vietnum, Brunei, Cambodia, Indonesia, Laos. Malaysia, Myanmar na Ufilipino.

XS
SM
MD
LG