Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 22:33

Mauaji ya Syria yajadiliwa UN

Kikao cha wajumbe katika baraza la usalama la umoja wa mataifa
Kikao cha wajumbe katika baraza la usalama la umoja wa mataifa

Utawala wa Assad hauelezei chochote juu ya tukio hilo, unaamini tu katika suluhisho la kijeshi, balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Samantha Power aliliambia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limefanya mazungumzo ya dharura Jumapili kuhusu ghasia za mauaji mabaya katika mji wa Aleppo wakati ndege za mapigano za Syria na Russia ziliposhambulia eneo la mashariki mwa mji wa Syria linalodhibitiwa na waasi.

Utawala wa Assad hauelezei chochote juu ya tukio hilo, unaamini tu katika suluhisho la kijeshi, balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Samantha Power aliliambia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Unasema unakwenda kudhibiti jeshi kila kona iliyobaki huko Syria, na haijali kile kilichobaki nchini humo katika kufanikisha hilo suluhisho la kijeshi.

Marekani, Ufaransa na Uingereza waliitisha kikao cha dharura kuishinikiza Russia kumdhibiti mshirika wake Syria ili kumaliza mashambulizi ya watu 275,000 waliokwama katika mji.

Mashambulizi ya makombora, mabomu na ufyatuaji maguruneti yameharibu majengo, na kuacha mitaa iliyojaa vifusi na mrundikano wa mabaki. Umoja wa mataifa unasema zaidi ya watu 213 wameuwawa katika mashambulizi hayo.

Balozi wa marekani katika Umoja wa Mataifa, Power, alisema zaidi ya mashambulizi ya anga 150 yalipiga katika mji katika siku tatu zilizopita, akiishutumu Russia na Syria kufanya mashambulizi hayo yote ili kuuteka tena mji wa Aleppo.

XS
SM
MD
LG