Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 07:23

2 wauwawa kwenye klabu ya usiku Marekani


Mtu mmoja ametiwa mbaroni baada ya tukio la ufyatuaji risasi kwenye klabu ya usiku katika jimbo la kusini mashariki mwa marekani la Florida na kusababisha vifo vya watu wawili.

Maafisa wanasema takriban watu 14 wamejeruhiwa na baadhi yao wakiwa katika hali mahututi, kutokana na tukio la jumatatu alfajiri nje ya klabu ya Blu huko Fort Myers Florida.

Polisi wamesema katika taarifa yao kwamba wananaendelea kufanya uchunguzi katika eneo hilo wakiangalia kama kuna watu wengine ambao wamehusika na tukio hilo.

Mwezi uliopita mauaji ya watu wengi yalifanyika katika klabu moja ya mashoga huko Orlando Florida na kupelekea kuuwawa kwa watu 49 na kwa mara nyingine tena kuweka suala la udhibiti wa bunduki kwenye kipaumbele cha uchaguzi mkuu wa 2016.

XS
SM
MD
LG