Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 03:15

Matokeo ya uchaguzi Burundi yazua hofu

Mwanamke wa Burundi akipiga kura yake katika uchaguzi wa bunge juni 29 , 2015
Mwanamke wa Burundi akipiga kura yake katika uchaguzi wa bunge juni 29 , 2015

Matokeo ya awali yalionyesha chama tawala cha rais Pierre Nkurunzinza kinaongoza kwa kuwa na kura nyingi na hakuna lililobadilika juu ya hilo.

Matokeo ya uchaguzi nchini Burundi bado hayajatolewa licha ya tume huru inayosimamia mchakato wa uchaguzi kusema kuwa yangetolewa mara baada ya upigaji kura wa juni 29.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika idhaa ya Kiswahili Haidalah Hakizimana anaripoti kuwa hakuna taarifa rasmi iliyotolewa Alhamisi ikieleza ni lini matokeo hayo yangetolewa.

Matokeo ya awali yalionyesha chama tawala cha rais Pierre Nkurunzinza kinaongoza kwa kuwa na kura nyingi na hakuna lililobadilika juu ya hilo.

kwa upande wa upinzani inasemeka uko kimya kwa vile tangu awali ulidai kususia uchaguzi huo, ingawa umeelekeza zaidi matumaini yake kwa jumuiya za kimataifa kusaidia katika mzozo wa kisiasa nchini Burundi.

Ghasia na mvutano wa kisiasa ulichochewa nchini Burundi baada ya rais Nkurunzinza kutangaza kugombea tena muhula wa tatu wa uongozi jambo lililopingwa na wapinzani wake wakidai kuwa ni kinyume cha katiba pamoja na makubaliano ya mkataba wa Arusha.

XS
SM
MD
LG