Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 15:03

Matembezi ya Kensa yafanyika Washington, DC


Maelfu wakishiriki katika matembezi ya kensa ya matiti Washington, D.C., June 4, 2011
Maelfu wakishiriki katika matembezi ya kensa ya matiti Washington, D.C., June 4, 2011

Timu ya Tanzania na nchi nyingine za Afrika zashiriki kuchangia katika harakati za kutafuta tiba ya kensa ya matiti

Maelfu kwa maelfu ya watu wakiwa wamevalia t-sheti za rangi ya waridi walijazana katika uwanja wa National Mall mjini Washington Jumamosi kushiriki katika matembezi ya kila mwaka ikiwa ni miongoni mwa juhudi za kampeni ya kupambana na kensa ya matiti.

Waandaaji wanakadiria kuwa kiasi cha watu elfu 40 walishiriki katika matembezi hayo ya kilomita tano kupitia katika maeneo kadha muhimu ya mjini Washington, umbali mfupi tu kutoka bunge la Marekani - U.S Capitol.

Miongozi wa waliohudhuria matembezi hayo ilikuwa timu ya Tanzania ambayo iliandaliwa na kina mama wa Kitanzania wanaoishi Washington, DC na maeneo ya jirani kumwunga mkono Dada Rehema Barksdale ambaye ametimiza miaka 10 tangu kupata tiba ya mafanikio baada ya kugundulika na kensa hiyo.

Barksdale anasifiwa katika jamii ya Watanzania kwenye eneo la Washington kwa ujasiri alionyesha katika juhudi za kuondoa unyanyapaa kwa wenye maradhi hayo na kuwahimiza wanawake na wasichana kuhakikisha wanapimwa mapema ili kupata tiba ya haraka endapo watakutwa na maradhi.

Matembezi kama hayo ya Washington yalifanyika pia katika miji kadha mingine nchini Marekani na sehemu nyingine duniani.

Mwanzilishi wa kampeni hiyo Nancy Brinker amesema fedha zinazopatikana katika kila matembezi zinatumika katika jamii hiyo hiyo, ikiwa ni pamoja na vipimo vya mapema na tiba.

XS
SM
MD
LG