Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 29, 2022 Local time: 08:47

Mataifa yamechelewa kuwasilisha ripoti kuhusu hali ya hewa-UN


Athari za mabadiliko ya hali ya hewa

Umoja wa Mataifa umesema kuwa mataifa mengi huenda yakachelewa kuwasilisha ripoti kuhusu udhibiti wa hali ya hewa mwaka huu, kama inavyohitajika kuambatana na mkataba wa Paris kutokana na janga la corona linaloendelea.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wiki iliopita alihimiza umuhimu wa kulinda hali ya hewa akisema wanadamu wako kwenye hatari ya kuangamiza mazingira.

Kwenye mkataba wa Paris uliotiwa saini 2015, mataifa yalikubaliana kudumisha viwango vya joto chini ya nyusi 2 Celcius, wakati shirika la Umoja wa Mataifa la UNDP, likisaidia mataifa 115 kati ya 197 yaliotia saini mkataba huo kuhakikisha kuwa hali ya heya inadhibitwa, mengi yakiwa maskini.

Mataifa hayo yanachangia karibu robo moja ya gesi inayotokana na greenhouse ulimwenguni yakiwemo Mexico na Nigeria. UNDP hata hivyo limesema kuwa huenda janga la Covid-19 likawa kizingiti cha mataifa mengi kuwasilisha ripoti zao kwa wakati.

Kufikia sasa, ni mataifa 8 pekee yalioko chini ya program ya UNDP, ambayo yamewasilisha ripoti zao yakiwemo Rwanda na Mongolia.

-Imetayarishwa na Harrison Kamau, VOA Washington DC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG