Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 04:15

Mataifa ya Ulaya kudumisha operesheni Mali kwa masharti mapya


Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Florence Parly alipokuwa akiondoka baada ya kushiriki katika mkutano wa kila wiki wa baraza la mawaziri katika Ikulu ya Rais ya Elysee huko Paris Julai 7. 2021.
Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Florence Parly alipokuwa akiondoka baada ya kushiriki katika mkutano wa kila wiki wa baraza la mawaziri katika Ikulu ya Rais ya Elysee huko Paris Julai 7. 2021.

Mataifa ya Ulaya yanayopambana na wanamgambo  wa Kiislamu nchini Mali yanasema yatajaribu kubuni njia ya kuendeleza misheni yao, lakini kuna viwango kwa gharama ambayo Ufaransa iko tayari kulipa ili kubaki huko, Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Florence Parly alisema siku ya  Jumamosi.

Akizungumza na shirika la habari la Reuters alisema uhusiano kati ya utawala wa kijeshi nchini Mali na washirika wake wa kimataifa unakaribia kuvunjika baada ya kushindwa kuandaa uchaguzi kufuatia mapinduzi mawili ya kijeshi.

Siku ya Jumatano, utawala huo wa kijeshi uliiambia Ufaransa ikome kuingilia kati masuala ya lililokuwa koloni lake na kukaa na matakwa yao ya kikoloni wao wenyewe.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian alisema Ijumaa kuwa hali iliyojitokeza haikutegemewa, kwani washirika wa Ulaya walikubali kuandaa mipango ndani ya wiki mbili ya jinsi ya kurekebisha kampeni zao, ambazo zinaijumuisha Mali na eneo kubwa la Sahel, kutokana na hali ya halisi ya mabadiliko.

Masharti ya kuingilia kati kwetu, iwe kijeshi, kiuchumi au kisiasa, yamekuwa magumu zaidi na magumu kuyadhibiti, Parly alisema.

Kwa kifupi, hatuko tayari kulipa gharama isiyo na kikomo ili kubaki nchini Mali.

Lakini alisema mawaziri kutoka nchi 15 zinazohusika na kikosi maalum cha Ulaya kwa sasa wameungana katika kudumisha operesheni hivyo lazima tuamue masharti yake mapya.

XS
SM
MD
LG