Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 30, 2024 Local time: 23:05

Masoko ya hisa ya Asia yashuka Jumanne


Masoko ya hisa barani Asia yalishuka Jumanne, huku hisa za benki zikiathirika zaidi, kufuatia kushuka kwa masoko ya Marekani huku kukiwa na anguko la benki mbili za Marekani.

Soko la hisa la Japan Nikkei lilishuka kwa asilimia 2, huku hisa za Softbank zikishuka kwa asilimia 4.1, Mizuho Financial Group ikishuka kwa asilimia 7.1, na Sumitomo Mitsui Financial Group ikiporomoka kwa asilimia 9.8. Soko la hisa la Hong Kong, Hang Seng lilifungwa likiwa na asilimia 2.4.

Rais wa Marekani, Joe Biden, Jumatatu alitaka kuwahakikishia Wamarekani kwamba mfumo wa benki wa Marekani upo salama na walipa kodi hawatatoa dhamana kwa wawekezaji wa Benki za Silicon Valley ya California na Signature Bank ya New York.

Alisema amana za wateja zitagharamiwa na fedha ambazo benki hulipa katika akaunti inayoshikiliwa na serikali ya Marekani kwa dharura kama hizo.

XS
SM
MD
LG