Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 17:24

Mashtaka ya mauwaji dhidi ya Mubarak yametupiliwa mbali


Mfuasi wa rais wa zamani Hosni Mubarak asherehkea nje ya hospitali ya kijeshi ya Maadi Cairo November 29, 2014.
Mfuasi wa rais wa zamani Hosni Mubarak asherehkea nje ya hospitali ya kijeshi ya Maadi Cairo November 29, 2014.

Jaji moja mjini Cairo atupilia mbali mashtaka dhidi ya rais wa zamani wa Misri, Hosni Mubarak kuhusiana na mauwaji ya waandamanaji wakati wa mapinduzi ya wananchi ya 2011 yaliyopelekea kuondolewa kwake madarakani.

Katika chumba cha mahakama kilichojaa watu hakimu Mahamoud Kamel al-Rashidi alisema, mashatka dhidi ya kongozi huyo aliyepinduliwa yamefutiliwa mbali na hayakulazimu hata hivyo kufikishwa mahakamani.

Watu walojaa ndani ya mahakama walishangiria kwa makelele uwamuzi huo. Vijana wa Mubarak na washtakiwa wenzake walimbusu kichwani alipokua anasikiliza uwamuzi kutoka kiti cha machera ndani ya chumba cha mahakama.

Kituo kimoja cha televisheni cha Misri kinaripoti kwamba mwendesha mashtaka anatafakari juu ya kupinga uwamuzi huo. Ripoti inaeleza kwamba mwendesha mashtaka anataka pia utafiti wa kisheria ufanyike juu ya sababu za kuchukuliwa uwamuzi huo.

Licha ya uwamuzi huo Mubarak atabaki katika kifungo cha nyumbani cha miaka mitatu akitumikia hukumu nyingine ya ubadhirifu wa mali ya umaa.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 86 aliyeongoza Misri kwa miongo mitatu alihukumiwa kifungo cha maisha mwaka 2012 kwa kuhusika na mauwaji ya waandamanaji. Hukumu hiyo ilibadilishwa na mahakama ya juu, kufuatia rufaa mwaka mmoja baadae na kesi mpya ikaanza tena. Tangu wakati huo Mubarak, amekuwa katika kifungo cha nyumbani katika hospitali ya kijeshi.

Uwamuzi wa Jumamosi unapelekea kuachiliwa huru waziri wake wa mambo ya ndani na washauri wake sita wa usalama.

Wafuasi wa Mubarak walokuwa nje ya mahakama walisherekea uwamuzi huo na kueleza furaha zao kutokana na uwamuzi huo. Naema Mohamed mfuasi wa kiongozi huyo.

Hakuna aneweza kukuondowa, wamisri wanakupenda kuanzia vijana hadi wazee kutoka walosoma hadi wasosoma tunakupenda sote tunakubaliana nawe.

wapinazni wa Mubarak wakiwa na hasira
wapinazni wa Mubarak wakiwa na hasira

Lakini wapinzani wa kiongozi huyo walieleza hasira zao, wakihisi juhudi zao za kuleta mageuzi nchini mwao zimekuwa za bure.

Katika kesi tofauti ya ulaji rushwa, mashtaka yalitupwa pia na Jaji Mahamoud Kamel al-Rashidi dhidi ya Mubarak na vijana wake Alaa na Gamal, akisema muda mrefu umepita tangu tuhuma za uhalifu huo kutokea kwa mahakama kuweza kuchukua uwamuzi juu ya suala hilo.

XS
SM
MD
LG