Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 12:18

Mashirika ya wanawake DRC yatetea kuorodheshwa kwao kwenye daftari la wagombea


Wanawake wa DRC na asasi za kiraia wataka wahusishwe zaidi katika uchaguzi na kuingizwa kwenye daftari la wagombea kwenye uchaguzi utakaofanyika mwakani.
Wanawake wa DRC na asasi za kiraia wataka wahusishwe zaidi katika uchaguzi na kuingizwa kwenye daftari la wagombea kwenye uchaguzi utakaofanyika mwakani.

Mwaka mmoja kabla ya uchaguzi nchini DRC, miungano ya wanawake inahoji kuhusu wanawake wenye nia yakuwa wagombea ambao hadi sasa hawajatiliwa maanani katika baadhi ya vyama vya kisiasa.

Nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, mwezi mmoja kabla kuanzishwa harakati za kuorodhesha wapiga kura ajili ya uchaguzi unaopangwa mwakani, baadhi ya mashirika ya wanawake yanatetea kuhusu kuorodheshwa kwa wanawake kwenye daftari la wagombea kwenye uchaguzi huo.

Wanasiasa wanasema ombi hili ni halali, ila asasi za kiraia zinaelezea changamoto zilizopo.

Mashirika hayo ya utetezi wa haki za wanawake yanashuhudia hofu kutokana na hali ya kwamba hadi sasa hakuna ishara dhahiri yoyote inayoonyesha kwamba vyama vya kisiasa vinajali wanawake wanaotarajia kugombea uchaguzi mwakani.

“Mwanamke wa kivu ya kusini anapenda kufanya siasa. Licha yakuwa kuna wanawake mashujaa wenye nia yakuwa wagombea, hawapewe fursa ya kuingia kwenye daftari za uchaguzi" anasema Solange Lwashiga Katibu Mtendaji wa jopo la wanawake ajili ya amani DRC.

Tangu mwanzo wa wiki hii, muungano wa wanawake katika upashaji habari mkoani Kivu Kusini AFEM unahamasisha wakazi kuhusu mabadiliko muhimu yaliyokusudiwa na sheria mpya ya uchaguzi nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, na umuhimu wake katika harakati za kuorodhesha wapiga kura.

Néné Bintu naibu kiongozi wa ofisi ya uratibu wa asasi za kiraia mkoani Kivu Kusini anasema Kuna shida ya mila, kulikuwa piana pingamizi kuhusu sheria ila nadhani kwa upande wa sheria mambo yametatuliwa. Huko DRC wanawake ni wengi ? Nadhani hawajaelewa kwamba wana uwezo wa kuwachagua wanawake wengine na kuwafikisha kwenye ngazi za uongozi

Katibu mtendaji wa tume huru ya uchaguzi mkoani Kivu kusini Gaudens Maheshe anabaini kuwa sheria ya uchaguzi inatilia maanani vijana, walemavu na haswa wanawake kuwa wagombea.

“Sheria inasema kuwa chama cha kisiasa au muungano wa kisiasa, unaoleta daftari yenye kuwa na asilimia hamsini ya wagombea wanawake hawatalipa pesa za ugombea. Inabaki kwa wanawake sasa, baada ya kuandikwa kwenye orodha ya wagombea, kujihakikisha sasa kwa wapiga kura, na kabla ya kuorodheshwa kuwa wagombea, inawabidi kuhakikishia vyama vyao vya kisiasa kwamba wana uwezo wa kufanya kazialisema Gaudens Maheshe, Katibu mtendaji wa CENI Kivu Kusini .

Tume ya uchaguzi nchini Congo - CENI inazidi kuhakikisha kwamba mnamo mwezi Desemba itaanzisha harakati za kuorodhesha wapiga kura. Waziri wa Fedha Nicolas Kazadi alisema CENI hadi mwezi Agosti iliyopita tayari imepokea zaidi ya dola milioni 400 za kimarekani kujiandaa kwa uchaguzi huo unaopangwa kufanyika mnamo mwaka 2023.

Imeandaliwa na Mitima Delachance, Sauti ya Amerika, Bukavu.

XS
SM
MD
LG