Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 07:46

Mashirika ya UN yanaonya kuongezeka kwa hali ya dharura ya chakula duniani


Baadhi ya kina mama wakiwa sokoni wanauza bidhaa mbalimbali huko kusini-magharibi mwa Nigeria. June 7, 2022.
Baadhi ya kina mama wakiwa sokoni wanauza bidhaa mbalimbali huko kusini-magharibi mwa Nigeria. June 7, 2022.

Nchi ya Sudan Kusini, Nigeria, Yemen na Afghanistan zipo katika viwango vya juu vya tahadhari kwa jamii ambazo tayari zinakabiliwa na njaa au zinabashiriwa na hatari ya kutumbukia katika njaa.

Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa yameonya Jumatatu juu ya kuongezeka kwa hali ya dharura ya chakula ikiwa ni pamoja na njaa nchini Sudan kutokana na kuzuka kwa vita na huko nchini Haiti, Burkina Faso na Mali kutokana na vizuizi vilivyowekwa kwa watu na bidhaa.

Nchi hizo nne zinaungana na Sudan Kusini, Nigeria, Yemen na Afghanistan, katika viwango vya juu vya tahadhari kwa jamii ambazo tayari zinakabiliwa na njaa au zinabashiriwa na hatari ya kutumbukia katika njaa.

Ripoti ya shirika la Chakula Duniani na Shirika la Chakula na Kilimo inahimiza tahadhari ya haraka ichukuliwe ili kuokoa maisha na ajira. Katika zaidi ya nchi hizo tisa zinazokadiriwa kiwango cha juu cha wasiwasi, mashirika hayo yalisema nchi 22 zinatambuliwa kama “maeneo makuu” yanayohatarisha usalama wa chakula.

Alitoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka katika sekta ya kilimo kuwaondoa watu kutoka kwenye ukingo wa njaa, kuwasaidia kujenga upya maisha yao na kutoa suluhisho la muda mrefu kushughulikia sababu za msingi za ukosefu wa chakula.

Forum

XS
SM
MD
LG