Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 10:24

Mashirika ya kiraia yasitisha shughuli zake Afghanistan


Wanawake wa Afghanistan wakiandamana kupinga marufuku ya wanawake kusoma vyuo vya elimu ya juu na kazi mjini Kabul Desemba 22, 2022.
Wanawake wa Afghanistan wakiandamana kupinga marufuku ya wanawake kusoma vyuo vya elimu ya juu na kazi mjini Kabul Desemba 22, 2022.

Mashirika kadhaa makubwa ya kigeni yasiyo ya kiserikali, au NGOs, nchini Afghanistan yalisimamisha programu za kibinadamu Jumapili, siku moja baada ya Taliban kuwazuia kuajiri wafanyakazi wanawake. 

Taarifa ya pamoja ya taasisi za Baraza la Wakimbizi la Norway (NRC), Save the Children na CARE International, ilisema kwamba mashirika yao hayawezi kufikia kwa ufanisi watoto, wanawake na wanaume walio na mahitaji makubwa nchini Afghanistan bila wafanyakazi wao wa kike.

Viongozi wa taasisi hizo walionya marufuku ya Taliban itaathiri utoaji wa msaada wa kuokoa maisha kwa mamilioni ya Waafghan na kuathiri maelfu ya kazi wakati wa mgogoro mkubwa wa kiuchumi unaoikabili nchi hiyo maskini.

Mashirika hayo matatu yasiyo ya kiserikali yanaendesha programu muhimu za afya, elimu, ulinzi wa watoto na lishe katika nchi hiyo iliyokumbwa na migogoro ambapo Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya nusu ya watu wanaokadiriwa kufikia milioni 40 wanahitaji aina fulani ya misaada ya kibinadamu.

Kando, Kamati ya Kimataifa ya Uokoaji (IRC) ilisema Jumapili ilikuwa inasimamisha shughuli za kibinadamu za Afghanistan, ikisema uwezo wake wa kutoa huduma unategemea wafanyakazi wa kike katika ngazi zote za shirika.

XS
SM
MD
LG