Vita kati ya jeshi la serikali na kundi la kijeshi la Rapid Support Forces, RSF, vimeacha karibu nusu ya wakazi milioni 49 wa Sudan, wakiwa kwenye hali ya kuhitaji misaada. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, zaidi ya watu milioni 7.5 wametoroka makwao, na kwa hivyo kufanya taifa hilo kuongoza ulimwenguni katika idadi ya watu waliotoroka makwao.
Kumekuwa na ripoti za misaada kuibwa, pamoja na kushambuliwa kwa wafanyakazi wa misaada, wakati mashirika ya kimataifa ya kutoa misaada yakilalamika kuhusu vizingiti vilivyoko kweye bandari ya Port Sudan, inayodhibitiwa na jeshi, wakati wakijaribu kufikisha misaada kwenye sehemu nyingine za nchi.
Forum