Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 24, 2020 Local time: 15:04

Mashirika ya haki za binadamu yaahirisha maandamano Malawi.


Mmoja wa waandamanaji akichoma majani barabarani huko Lilongwe Malawi.

Mashirika ya haki za binadamu yaahirisha maandamano lakini yaonya maandamano kuanza tena ikiwa rais hatojibu matakwa yao.

Mashirika ya haki za binadamu Malawi yameahirisha maandamano ya kitaifa ya kupinga serikali yaliokuwa yamepangwa wiki hii, wakisema wanangojea matokeo ya rufaa dhidi ya mpango wao.

Msemaji wa makundi ya haki za binadamu Rogers Newa aliuambia mkutano wa waandishi wa habari leo kuwa mahakama kuu linatafakari juu ya mashtaka ya wafuasi wa serikali kutaka kuzuia maandamano ya upinzani.

Newa anasema wanaharakati wa haki za binadam wa Malawi wanataka kuruhusu kesi hiyo na juhudi za usuluhishi kuendelea. Wanaharakati walikuwa wamepanga kuanza maandamano kesho ikiwa rais Bingu wa Mutharika hatojibu matakwa yao. Hakuna tarehe mpya iliyotangazwa kwa maandamano hayo.

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG