Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 05, 2024 Local time: 06:14

Mashirika ya habari ya Tanzania na Comoro yataka ushirikiano baina yao


Kampeni ya uchaguzi visiwani Comoros
Kampeni ya uchaguzi visiwani Comoros

Ujumbe huo umetiliana saini mikataba ya ushirikiano katika maeneo mbalimbali siku ya jumatano

Ujumbe wa wakurugenzi kutoka shirika la habari la Tanzania la TBC, na ule wa shirika la utangazaji la Zanzibar umefanya ziara maalumu visiwani Comoro katika kile kinachodaiwa ni kuboresha ushirikiano wa nchi hizo.

Ujumbe huo umetiliana saini mikataba ya ushirikiano katika maeneo mbalimbali siku ya jumatano na shirika la habari la Radio na Televisheni la Comoro ikiwa ni pamoja na ubadilishanaji wa vipindi na kukuza lugha ya Kiswahili.

Wajumbe waliohudhuria katika utiaji saini huo ni pamoja na mkurugenzi wa shirika la habari la Tanzania la TBC, bwana Clement Mshana , mkurugenzi wa shirika la habari la utangazaji la Zanzibar bwana Mohamed Mitawi na mkurugenzi wa shirika la habari la utangazaji Comoro bwana Saleh Mohamed Saleh.

Katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari wakurugenzi hao walisisitiza kuwepo na utamaduni ulioungana kati ya nchi husika katika ubadilishanaji wa vipindi vitakavyoleta manufaa katika nchi hizo na hata kubadilishana wafanyakazi wa mashirika hayo.

Akizungumza katika mkutano huo mkurugenzi wa TBC, bwana Mshana alisema nia ya dhati ni kuendeleza ushirikiano baina ya mashirika na nchi hizo katika mwaswala ya habari, burudani ikiwa ni pamoja na nyimbo na michezo.

Pia wakurugenzi hao wamesema mashirika yao yamekubaliana kuonesha mechi za mpira za kimataifa za nchi hizo na kuonesha tamaduni zake na hata kutoa mafunzo kwa watangazaji wake.

XS
SM
MD
LG