Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 04, 2024 Local time: 00:55

Mashambulizi ya Ukraine nchini Russia yameua watu wawili


Mabaki baada ya shambulizi latika mji wa Belgorod nchini Russia
Mabaki baada ya shambulizi latika mji wa Belgorod nchini Russia

Ni jaribio la karibuni katika mapambano ya makombora ya masafa marefu na ufyatuaji roketi katika vita vya Russia kwa Ukraine

Mashambulizi ya Ukraine katika mji wa Belgorod nchini Russia, karibu na mpaka wa Ukraine, yamewaua watu wawili, maafisa wa Russia wamesema Jumamosi. Mwanamme na mwanamke mmoja walifariki katika shambulizi na watu wengine watatu wamejeruhiwa, Gavana wa mkoa Vyacheslav Gladkov amesema katika mtandao wa Telegram.

Ilikuwa ni jaribio la hivi karibuni katika mapambano ya makombora ya masafa marefu na ufyatuaji wa roketi katika vita vya Russia kwa Ukraine. Watu watano pia walijeruhiwa wakati ndege isiyo na rubani ya Ukraine ilipopiga gari katika kijiji cha Glotovo, kilomita 2 kutoka mpaka wa Ukraine, Gladkov alisema.

Pia leo Jumamosi shambulio la ndege isiyo na rubani ya Ukraine lilisababisha moto katika kiwanda cha kusafisha mafuta cha kampuni kubwa ya mafuta ya Russia ya Rosneft katika mkoa wa Samara, Gavana wa mkoa Dmitry Azarov alisema. Alisema kuwa shambulio dhidi ya kiwanda kingine cha kusafisha mafuta lilizimwa. Hakuna vifo vilivyoripotiwa.

Forum

XS
SM
MD
LG