Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 18:23
VOA Direct Packages

Mashambulizi pamoja na uporaji wa mali zaripotiwa kwenye eneo la Darfur, Sudan, licha ya sitisho la muda la mapigano


Wanajeshi kutoka kikosi cha kijeshi cha RSF nchini Sudan.
Wanajeshi kutoka kikosi cha kijeshi cha RSF nchini Sudan.

Wapiganaji wenye silaha kweye eneo la Sudan lililotatizwa  na mapigano la Darfur, Alhamisi wamefanya mashambulizi huku pia wakipora mali kwenye maduka na nyumba za watu kulingana na wakazi.

Hilo limetokea licha ya sitisho la amani na muda lililofikiwa kati ya majenerali wawili wakuu wa taifa hilo, ambao mivutano ya madaraka kati yao imesababisha vifo vya mamia ya watu ndani ya siku kadhaa zilizopita. Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, ghasia zilizoshuhudiwa kwenye mji wa Darfur wa Genena. zinadhihirisha namna mivutano ya kudhibiti mji mkuu wa Khartoum inavyopelekea ghasia kwenye sehemu nyingine za Sudan.

Pande zinazozozana Alhamisi zilikubali kuongeza muda wa sitisho la mapigano kwa saa 72. Hata hivyo makubaliano hayo yalioongozwa na Marekani na Saudi Arabia hayajasitisha mapigano, lakini yametoa nafasi kwa maelfu ya raia kutorokea kwenye maeneo salama, pamoja na mataifa ya kigeni kuweza kuondoa raia wake kutoka nchini humo kwa njia za meli au barabara. Sitisho la mapigano linasemekana kuleta utulivu kwa kiasi fulani kwenye mji mkuu wa Khartoum pamoja na mji wa karibu wa Omdurman, kwa mara kwa kwanza tangu jeshi la serikali, na kundi hasimu la kijeshi la RSF kuanza mapigano Aprili 15, na kugeuza makazi ya watu kuwa uwanja wa vita.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, ambaye amekuwa akishauriana na majenerali wawili wanaoongoza pande zinazohasimiana awali alizungumzia kuhusu muda mfupi wa sitisho la mapigano, akisema kwamba angejitahidi kuona ukiongezwa. Wakati huo huo Ikulu ya Marekani imetoa wito kwa wamarekani waliyopo Sudan kuondoka nchini humo ndani ya saa 24 hadi 48. Hata hivyo kumekuwa na malalamishi kwamba Marekani imezembea katika kuokoa raia wake kwa haraka kama yanavyofanya mataifa mengine ya kigeni.

XS
SM
MD
LG