Mashabiki wa timu ya Mexico wameendelea kusheherekea ushindi wao dhidi ya bingwa mtetezi wa Kombe la Dunia, Ujerumani, baada ya kuifunga goli (1 - 0) katika mchezo wao wa awali katika michuano hiyo.
Kwa upande wa mashabiki wa Ujerumani, wao wamesikitishwa na matokeo hayo na kueleza kwamba timu yao haikucheza mchezo mzuri waliotarajia.