Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 02:58

Leo ni sikukuu ya MLK Marekani


Martin Luther King Jr akihutubia.
Martin Luther King Jr akihutubia.

King alianza kupata umaarufu mwaka wa 1955 alipoongoza maandamano ya kususia usafiri wa umma kwenye mabasi mjini Montgomerry, Alabama, huku akipinga ubaguzi wa rangi uliokuwa umekithiri.

Wamarekani kote nchini hii leo wameendelea kuadhimisha sikukuu ya kuzaliwa kwa kiongozi wa kutetea haki za binadamu hapa Marekani Martin Luther King jnr, aliyeuawa mwaka 1968.

King alianza kupata umaarufu mwaka wa 1955 alipoongoza maandamano ya kususia usafiri wa umma kwenye mabasi mjini Montgomerry, Alabama, huku akipinga ubaguzi wa rangi uliokuwa umekithiri. Mgomo huo ulifaulu kwa kisitisha ubaguzi uliowalenga wamarekani weusi. King aliibuka kama kiongozi mkuu wa harakati za kutetea haki za binadamu katika miaka ya hamsini na sitini.

Aliwapa wengi matumaini kwa hotuba yake maarufu ya I HAVE A DREAM yaani “nina Ndoto” aliyoitoa mwaka wa 1963. Kiongozi huyo alipata tuzo la Nobel mnamo mwaka wa 1964, wakati ambapo rais wa wakati huo Lyndon Johnson alitia saini mswada muhimu wa haki za binadamu. King aliuawa tarehe 4, Aprili mwaka 1968 mjini Memphis, Tennessee alipokuwa anajiunga na wafanyakazi weusi wa kuzoa taka ambao walikuwa wakiandamana kudai malipo nafuu

XS
SM
MD
LG