Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 08:34

Marekani yawawekea vikwazo washirika wa Rais Kabila wa DRC


Ghasia za kisiasa nchini DRC
Ghasia za kisiasa nchini DRC

Marekani Jumatano iliwawekea vikwazo wafanyakazi wawili wa karibu na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC, Joseph kabila kwa sababu ya kudumaza demokrasia na kukandamiza uhuru wa kujieleza na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Aidha mali za wafanyakazi hao zilizopo nchini Marekani zimezuiliwa na pia raia wa marekani wamezuiwa kufanya biashara na watu hao. Majina ya maafisa hao wawili waliowekewa vikwazo ni Meja Jenerali Gabriel Amisi Kumba na mkuu wa zamani wa polisi John Numbi ambaye ni mmoja wa washauri waandamizi wa bwana Kabila.

Jengo la White House
Jengo la White House

Maafisa wa Marekani walisema Numbi alitishia kuwauwa wagombea wa upinzani ambao walikataa kujitoa kwenye uchaguzi mdogo mwezi Machi na wanamshutumu Kumba kuongoza kitengo cha jeshi ambacho kilifanya ghasia na kutumia nguvu kupita kiasi dhisi ya waandamanaji wa kisiasa.

Watu wengi nchini DRC walisema Kabila na washirika wake wanatumia ghasia na ukandamizaji kujaribu kushikilia madaraka.

XS
SM
MD
LG