Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 23, 2024 Local time: 02:26

Marekani yawawekea vikwazo viongozi saba waandamizi wa Iran


Rais wa Iran Ebrahim Raisi alipohudhuria mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran, Iran Agosti 29, 2022. Majid Asgaripour/WANA
Rais wa Iran Ebrahim Raisi alipohudhuria mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran, Iran Agosti 29, 2022. Majid Asgaripour/WANA

Marekani Alhamisi iliwawekea vikwazo viongozi saba waandamizi wa Iran kwa jukumu lao la kuzima mtandao wa intaneti nchini humo na msako unaoendelea dhidi ya wapinzani .

Wapinzani hao wanaopinga kifo cha msichana mdogo aliyekuwa chini ya ulinzi wa polisi wa maadili wa nchi hiyo kwa kushindwa kufunika nywele zake ipasavyo kwa hijabu.

Wizara ya Fedha ilimlenga Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran Ahmad Vahidi, na waziri wa mawasiliano wa nchi hiyo, Eisa Zarepour, pamoja na maafisa wengine watano katika vyombo vya usalama vya Iran.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema katika taarifa yake kwamba "Marekani inalaani kitendo cha serikali ya Iran kuendelea kukandamiza maandamano kufuatia kifo cha kutisha cha Mahsa Amini mwenye umri wa miaka 22 chini ya ulinzi wa polisi wanaojiita polisi wa maadili. tangu kukandamiza haki ya uhuru wa kujieleza na haki ya kukusanyika kwa amani."

Naibu waziri wa Fedha Brian Nelson alisema, "Haki za uhuru wa kujieleza na kukusanyika kwa amani ni muhimu katika kuhakikisha uhuru na utu wa mtu binafsi. Marekani inalaani kitendo cha serikali ya Iran kuzima mtandao na kuendelea kukandamiza maandamano ya amani na haitasita kufanya hivyo. kuwalenga wale wanaoelekeza na kuunga mkono vitendo hivyo.

XS
SM
MD
LG