Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 16:36

Marekani yatupia jicho ushirika na Sudan


Nembo ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani
Nembo ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani

Utawala wa Obama ambao umeafikiana urafiki mpya na nchi kama Cuba, Iran na Myanmar hivi sasa unatupia jicho kufikia makubaliano na nchi ya Sudan ambayo kwa muda mrefu imeonekana taifa linalofadhili ugaidi na ambapo kiongozi wake aliyepo madarakani amefunguliwa mashtaka ya uhalifu wa vita.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated press-AP wakati mabadiliko mbadala ya sera za Marekani kwa Sudan hayaonekani kutokea hivi karibuni wizara ya mambo ya nje ya Marekani Jumanne ilikaribisha ushirikiano wa Khartoum katika mapambano na kundi lenye msimamo mkali la Islamic State-IS.

Ramani ya Sudan
Ramani ya Sudan

Taarifa ambayo haikueleza kinaga ubaga juu ya maendeleo hayo ilisema Sudan katika miezi ya karibuni ilichukua hatua muhimu ya kukabiliana na kundi la Islamic State pamoja na mitandao mingine kama hiyo. Iliongeza kwamba Marekani itafanya kazi na Sudan kwenye masuala ya usalama huku pia ikiishinikiza kwenye masuala yake ya haki za binadamu na demokrasia.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani Marekani, John Kirby alisema Marekani inaendelea kuwa na wasi wasi mkubwa kuhusu sera za Sudan ikielezea ghasia huko magharibi mwa mkoa wa Darfur.

XS
SM
MD
LG