Marekani inawaonya raia wake waliopo Nigeria kwamba kundi la ki-Islam lenye msimamo mkali la Boko haram huwenda linapanga mashambulizi katika mji mkuu, Abuja.
Ubalozi wa marekani umetoa ujumbe wa dharura ukisema mashambulizi yanaweza kulenga mahoteli yanayotumiwa na mataifa ya magharibi, lakini muda wa mashambulizi haujulikani.
Onyo hilo limesema serikali ya Nigeria inafahamu juu ya kitisho hicho na kwa sasa imeongeza kiwango cha usalama.
Ubalozi umewatahadharisha raia kuwa makini na usalama wao katika maeneo ya karibu na majengo ya serikali ya Nigeria, ubalozi, na mahala penye mikusanyiko mikubwa, masoko na sehemu za ibada.