Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 30, 2023 Local time: 01:09

Marekani yatenga dola bilioni 10 kwa Taiwan katika bajeti yake ya ulinzi


Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen akikutana wabunge wa Marekani mjini Taipei, Septemba 8, 2022.

Baraza la Wawakilishi la Marekani Alhamisi limepitisha mswaada wa matumizi ya ulinzi ambao unajumuisha mpaka dola bilioni 10 za msaada wa kijeshi kwa Taiwan na kutaka kuharakisha uuzaji wa silaha kwa kisiwa hicho, hatua ambayo imekemewa na Beijing.

Mswaada huo wa ulinzi kwa mwaka 2023 ambao unahitaji kuidhinishwa na Baraza la Seneti na kusainiwa na Rais Joe Biden ili kuwa sheria, utaruhusu utoaji wa msaada kwa Taiwan hadi dola bilioni 2 kwa mwaka kuanzia mwaka 2023 hadi 2027.

Mswaada huo unamruhusu Biden kutoa hadi dola bilioni 1 kwa mwaka kama msaada wa vifaa vya kijeshi kutoka Marekani au huduma nyinginezo kama vile mafunzo ya kijeshi.

Beijing “imekuwa ikipinga vikali Marekani kutumia sheria ya taifa ya ulinzi kwa kupitisha maudhui mabaya kuhusiana na China,“ msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Mao Ching aliwaambia waandishi wa habari baada ya mswaada huo kupitishwa.

Beijing inadai Taiwan ni sehemu ya ardhi yake, ambayo itaunganishwa siku moja kwa nguvu, ikiwa itahitajika.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG