Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 28, 2020 Local time: 08:21

Marekani yatekeleza ahadi yake Cameroon

watu waliotoroka makazi yao nchini Cmeroon wakiwa katika kambi ya wakimbizi ya Minawao

Mkuu wa komandi ya Marekani katika masuala ya Afrika David Rodriguez amesema karibu wanajeshi 90 kati ya 300 walioahidiwa na Marekani wako njiani kwenda Cameroon .

Marekani imetuma vifaa na kiasi kadhaa cha wanajeshi nchini Cameroon kwa ajili ya kupambana na ugaidi wa kundi la Boko Haram.

Mkuu wa komandi ya Marekani katika masuala ya Afrika David Rodriguez amesema karibu wanajeshi 90 kati ya 300 walioahidiwa na Marekani wako njiani kwenda Cameroon .

Miongoni mwa vifaa vilivyopelekwa nchini humo ni pamoja na magari yenye silaha nzito yenye uwezo wa kutambua mabomu ya kutegwa ardhini. Kanali Jean Jacques Fouda ambaye ni kiongozi wa vifaa vya kijeshi nchini Cameroon hayajaweka bayana idadi kamili ya vifaa lakini amesema magari yenye silaha nzito ni muhimu sana ikilinganishwa na yale nchi hiyo iliyokuwa nayo.

Anasema yanauwezo wa kulinda wanajeshi katika doria, kufanya operesheni za masafa marefu na kupambana na mabomu hasa ya kutegwa ardhini.

Wiki hii Marekani ilitangaza ilikuwa inatuma wanajeshi 300 kupambana na ugaidi nchini Cameroon.

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG