Kuna mateka kadhaa wanaendelea kushikiliwa Gaza, na wanasubiri makubaliano ambayo yatawarudisha nyumbani.
“Ni wakati wa kukamilisha mpango huo,” msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Matthew Miller, amewaambia wanahabari baada ya vikosi vya Israel kuwapata mateka sita mwishoni mwa juma waliokuwa chini Hamas wamekufa kwenye handaki katika mji wa Rafah kusini mwa Gaza.
Amesema Marekani itafanya kazi katika siku zijazo na wapatanishi Misri na Qatar kuongeza kasi ya makubaliano ya mwisho. Jambo moja kuu la mzozo katika mazungumzo hayo ni kusisitiza kwa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kwamba wanajeshi wa Israel, wabaki kwenye mpaka kati ya Gaza na Misri.
Forum