Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 09:35

Marekani yasitisha zoezi la kijeshi na Uganda


Mwanajeshi wa kikosi maalumu cha jeshi la Marekani akiwa katika zoezi la kikanda barani Afrika
Mwanajeshi wa kikosi maalumu cha jeshi la Marekani akiwa katika zoezi la kikanda barani Afrika
Marekani imefuta zoezi la kijeshi la kikanda lililopangwa kufanyika Uganda ikiwa ni moja wapo ya misaada inayositishwa kwa taifa hilo la Afrika mashariki katika kujibu sheria mpya ya nchi hiyo inayopiga marufuku vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.

Utawala wa Obama ulitangaza Alhamis kwamba hatua hizo ziliwalenga wale wanaowajibika na unyanyasaji unaohusiana na sheria dhidi ya mashoga vile vile dhidi ya maafisa wa Uganda waliokutwa na hatia ya ulaji rushwa mkubwa wa mali ya umaa.

Zaidi ya kusitisha zoezi la jeshi la anga ambalo kituo cha kijeshi cha Marekani kwa ajili ya afrika kilibidi kukutana na majeshi ya Uganda baadae mwaka huu. Hatua iliyotangazwa Alhamis itapunguza viza ya kuingia Marekani na kusitisha au kuhamisha fedha za kugharimia miradi mbali mbali ya afya ya umma na usalama.

Hata hivyo maafisa wa Marekani walisema hatua hizo hazita-athiri moja kwa moja msaada wa chakula na miradi ya msaada kwa Waganda wanaoishi na virusi vya HIV au Ukimwi.

Msemaji wa baraza la usalama wa kitaifa kwenye White House, Caitlin Hayden alisema vikwazo vipya vinaongeza juhudi za Marekani zilizoanza mwezi April za kupinga sheria ya kupinga tabia ya ushoga iliyotiwa saini na Rais Yoweri Museveni ambayo inatoa kifungo cha maisha jela kwa kile kinachoitwa, mashoga wanaokaidi.

Maafisa walisema baadhi ya maafisa wa Uganda wale waliohusika katika unyanyasaji mbaya wa haki za binadamu ikiwa ni pamoja na vitendo dhidi ya mashoga watapigwa marufuku kusafiri kuingia Marekani.
XS
SM
MD
LG