Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 03, 2024 Local time: 20:57

Marekani yasema pande zote za mgogoro wa Sudan zimefanya uhalifu wa kivita


Marekani, Jumatano imesema vikosi hasimu vya Sudan vyote vimefanya uhalifu wa kivita katika mzozo wao na kudaiwa kuanzisha kampeni mpya ya mashambulizi ya kikabila katika eneo lenye kumbukumbu ya maafa la Darfur.

Baada ya miezi kadhaa ya wasiwasi na kushindikana kwa mazungumzo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken aliwasilisha matokeo kufuatia tathmini ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani.

Waziri Blinken, amesema jeshi la Sudan na vikosi vya akiba vya RSF, ambavyo mvutano wao wa muda mrefu ulikuwa na kusababisha ghasia kubwa Aprili 15, vimefanya uhalifu wa kivita.

RSF pia imefanya mauaji ya kikabila na uhalifu dhidi ya ubinadamu, amesema, akizungumzia mauaji ya kimbari yaliyofanywa na kikosi kikubwa cha Waarabu na wanamgambo washirika wake dhidi ya watu wa kabila la kiafrika la Masalit huko Darfur.

Forum

XS
SM
MD
LG